01. Hadiyth “Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na elimi… “

123- Zayd bin Arqam (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipenda kusema:

اللهم إني أعوذ بك من علم لا ينفع ومن قلب لا يخشع ومن نفس لا تشبع ومن دعوة لا يستجاب لها

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na elimi isiyonufaisha, kutokamana na moyo usionyenyekea, kutokamana na nafsi isiyoshiba na kutokamana na du´aa isiyojibiwa.”[1]

Ameipokea Muslim, at-Tirmidhiy na an-Nasaa´iy.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/161)
  • Imechapishwa: 05/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy