01. Hadiyth “Atakayetawadha, akaweka vizuri wudhuu´ wake, kisha akaenda ijumaa… “

683- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Atakayetawadha, akaweka vizuri wudhuu´ wake, kisha akaenda ijumaa, akasikiliza na kunyamaza, basi anasamehewa yaliyoko kati yake na ijumaa ijayo na ukiongezea na siku tatu. Na yule atakayegusa kokoto basi amefanya upuuzi.”

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah[1].

Kuhusiana na kufanya upuuzi, imesemekana kuwa amekosa ujira. Kuna maoni mengine yenye kusema kuwa amekosea. Kuna maoni mengine yanayosema kuwa ijumaa yake imekuwa Dhuhr. Kumesema mengine yasiyokuwa hayo[2].

[1] Swahiyh. Imepokelewa vilevile na Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” (1762) kupitia kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ameongeza:

”Abu Hurayrah amesema: ”Ukiongezea siku tatu. Allaah analipa tendo jema kwa kumi mfano wake.”

Imepokelewa katika ”as-Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (370). Nyongeza hii imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Abu Maalik al-Ash´ariy. Itakuja baada ya Hadiyth hii na kupitia kwa Ibn ´Amr.

[2] Kutokana na Hadiyth inayofuata maoni sahihi ni haya ya mwisho. Hata hivyo hayapingani na maoni mengine yaliyotolewa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/430)
  • Imechapishwa: 06/01/2017