Kazi ya mwanamke katika kuitengeneza jamii ina umuhimu mkubwa. Hilo ni kwa kuwa kuitengeneza jamii kunakuwa kwa aina mbili:

Aina ya kwanza: Utengenezaji wa dhahiri. Huu ni ule utengenezaji unaokuwa masokoni, misikitini na kwenginepo katika mambo ya dhahiri. Uwanja huu umeshikwa na wanaume wengine. Kwa kuwa wao ndio wako wazi na ndio wenye kuonekana.

Aina ya pili: Kuitengeneza jamii nyuma ya kuta. Hili linakuwa katika manyumba. Umuhimu wake mkubwa unamwelekea mwanamke kwa dhati yake. Mwanamke ndiye mama wa nyumba. Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akiwazungumzisha wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا

“Tulizaneni majumbani mwenu na wala msionyeshe mapambo kama walivyokuwa wakifanya watu wa jaahiliyah wa mwanzo na simamisheni swalah na toeni zakaah na mtiini Allaah na Mtume Wake. Hakika Allaah anataka akuondosheeni maovu, enyi ahli wa nyumba na akutakaseni mtakaso kisawasawa.”[1]

[1] 33:33

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017