00. Dibaji ya Shaykh Swaalih al-Fawzaan


Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Amma ba´d:

Huu ni ufupisho wa “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kutoka katika vyanzo vifuatavyo:

1- “Rawdhwat-un-Nadiyyah Sharh al-´Aqiydat-il-Waasitwiyyah” ya Shaykh Zayd bin ´Abdil-´Aziyz bin Fiyaadhw.

2- “at-Tanbiyhaat-us-Sunniyyah ´alaa al-´Aqiydat-il-Waasitwiyyah” ya Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Naaswir ar-Rashiyd.

3- “at-Tanbiyhaat-il-Latwiyfah fiymaa ihtawatw ´alayh al-Waasitwiyyah min al-Mabaahith al-Maniyf” ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy.

4- Nukuu za faida nilizoziwekea taaliki kwenye nuskha yangu wakati wa maombi.

5- Kuhusiana na yale yanayohusiana na kufasiri Aayah nimenukuu kutoka katika vitabu vya Tafsiyr ya Qur-aan kama mfano wa “Fath-ul-Qadiyr” ya Imaam Muhammad bin ´Aliy ash-Shawkaaniy na “Tafsiyr-ul-Qur-aan al-´Adhwiym” ya Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr.

Chuo kikuu cha Kiislamu cha Imaam Muhammad bin Su´uud kilikuwa kimekichapisha mara nyingi na kukieneza kwa wanafunzi ambao wako katika ngazi ya sekondari. Namshukuru Allaah kwa wale waliosimamia kazi hiyo na Allaah awazidishie kheri na mafanikio kwa yale yaliyo na kuwatengeneza waislamu. Vilevile namuomba Allaah anufaishe kwacho na akijaalie kiwe kimefikia lengo la kuiweka wazi ´Aqiydah hii tukufu, anisamehe yale makosa nitayokuwa nimetumbukia ndani yake na anithibitishe kwa yale ya sawa yaliyomo ndani yake. Kwani hakika Yeye ni Mwing wa kusikia, Mwenye kuitika.

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wake. Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 02
  • Imechapishwa: 07/02/2018