Himdi zote njema ni Zake Allaah Mmoja pekee na swalah na salamu zimwendee yule ambaye hakuna Nabii mwengine baada yake.

Wa ba´d:

Muhadhara huu niliutoa kwa wanafunzi wa Daar-ul-Hadiyth Makkah mwaka wa 1401 H kwa anuani ”Uhakika wa Suufiyyah katika mwanga wa Qur-aan na Sunnah”. Baada ya hapo walipendekeza baadhi ya watenda kheri kukichapisha na kukieneza ili faida iweze kuenea na nikakubali hilo pamoja na ufinyu wa wakati. Wakati nilipokuwa naiandaa, nilifikiria upeo wa uelewa kwa wale wanafunzi ambao niliwatolea muhadhara huu na kwa ajili hiyo ndio maana ukawa ni sahali kuuelewa na wakati huohuo ukawa unahusiana na maudhui mbalimbali – na himdi zote ni Zake Allaah. Ninamuomba Allaah (Ta´ala) awanufaishe nao kila yule ambaye ni mtafutaji wa haki. Hakika Allaah ni Mjuzi zaidi wa nia zetu.

Imeandikwa na:

Muhammad bin Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy

Makkah

6/3/1404

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqat-us-Suufiyyah
  • Imechapishwa: 10/12/2019