01. Utangulizi wa “Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam”


بسم الله الرحمن الرحیم

Himdi zote anastahiki Allaah. Tunamhimidi Yeye na kumuomba msaada na msamaha. Tunajilinda Kwake kutokamana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Hakika yule aliyeongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na yule aliyepotezwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Allaah amswalie yeye, kizazi chake na Maswahabah wake.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa nyinyi [mmeshakuwa] ni Waislamu.” (03:102)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja na Akaumba kutoka humo mke wake na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana na jamaa. Hakika Allaah Amekuwa juu yenu ni Mwenye kuchunga.” (04:01)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا

“Enyi mlaomini! Mcheni Allaah na semeni kauli ya kweli [ya sawasawa]. Atakutengenezeeni ‘amali zenu na Kukusameheeni madhambi yenu; na anayemtii Allaah na Mtume Wake, basi kwa yakini amefanikiwa mafaniko adhimu.” (33:70-71)

Hakika maneno ya kweli kabisa ni Kitabu cha Allaah na uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mambo maovu kabisa ni yale ya kuzua. Kwa kuwa kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu na kila upotevu ni Motoni.

Amma ba´d:

Nitazungumzia baadhi ya Aayah kutoka katika Suurah “al-Baqarah”, nazo ni zile Aayah ambazo Allaah ametufaradhishia kupitia kwazo swawm na akataja baadhi ya hukumu zake. Ninamuomba Allaah kwa unyenyekevu ajaalie kazi hii iwe imefanywa kwa ajili Yake pekee na amnufaishe nayo na kumpa faida yule (Subhaanah) Anayemtaka.

Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba msamaha kwa yale nisiyoyajua. Hakika Wewe unajua na mimi sijui. Hakika Wewe ndiye mjuzi wa yaliyofichikana. Ee Allaah! Nitunuku uwerevu na unilinde na shari ya nafsi yangu. Ee Allaah! Hakika mimi najitenga mbali kutokamana na nguvu na uwezo wa nafsi yangu na ninatambua nguvu na uwezo Wako.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 6-7
  • Imechapishwa: 02/06/2017