Swali: Kuna mtu anayelingania na kuamrisha mema na kukataza mabaya, lakini hasikilizwi. Nini nasaha yenu kwake?
Jibu: Hilo halitomdhuru. Lakini inampasa atafute njia yenye manufaa, kwani nakhofia kuwa kutoleta manufaa kunatokana na ubaya wa njia yake, ukali wake na ghadhabu yake. Hivyo abadili njia yake na aangalie sababu za kutoleta manufaa. Ni lazima ajipime nafsi yake; huenda ni mwenye maasi na hivyo watu wanamdharau kwa sababu ni mwenye maasi. Anasema lakini hatendi. Hii ni sababu mbaya na kubwa. Au huenda hajui njia nzuri ya ulinganizi au kwa sababu nyinginezo. Hivyo aangalie na ajipime nafsi yake na amche Allaah. Hakika hafanikiwi isipokuwa kwa sababu ya dhambi katika dhambi zake, jambo ambalo mara nyingi ndilo hutokea. Huenda pia akawa hasikilizwi hata kama ni mtengemavu zaidi ya watu, lakini aihesabu na kuiangalia nafsi yake. Akiuona upungufu au kosa alitibu, na asipoona kitu basi ni vyema na hilo halitomdhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikaa Makkah muda mrefu – miaka kumi na tatu – lakini waliomkubali walikuwa wachache tu. Hata hivyo hilo halikumdhuru. Kama mlivyosikia katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas ambaye amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Nilionyeshwa ummah na nikamwona Mtume akiwa na kundi dogo.”
Imekuja kaktika riwaya ya Muslim:
”… kundi dogo la watatu, wanne au watano. Mtume mwingine akiwa na mtu mmoja au wawili. Mtume mwingine bila mtu yeyote.”
Baadhi ya Manabii hakuna mtu hata mmoja aliyemtii kabisa. Hawakukubaliwa kutoka kwake. Bali walimuua. Atakuja siku ya Qiyaamah peke yake akiwa hana mtu yeyote katika ummah wake aliyemfuata. Lakini hilo halitomdhuru. Hata hivyo huyu atakuwa ametekeleza wajibu wake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29416/%D9%85%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%88%D8%AC%D9%8A%D9%87%C2%A0%D9%84%D9%85%D9%86-%D9%8A%D9%86%D8%B5%D8%AD-%D9%84%D9%84%D9%86%D8%A7%D8%B3-%D8%AF%D9%88%D9%86-%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D8%AC%D8%A7%D8%A8%D8%A9
- Imechapishwa: 10/08/2025
Swali: Kuna mtu anayelingania na kuamrisha mema na kukataza mabaya, lakini hasikilizwi. Nini nasaha yenu kwake?
Jibu: Hilo halitomdhuru. Lakini inampasa atafute njia yenye manufaa, kwani nakhofia kuwa kutoleta manufaa kunatokana na ubaya wa njia yake, ukali wake na ghadhabu yake. Hivyo abadili njia yake na aangalie sababu za kutoleta manufaa. Ni lazima ajipime nafsi yake; huenda ni mwenye maasi na hivyo watu wanamdharau kwa sababu ni mwenye maasi. Anasema lakini hatendi. Hii ni sababu mbaya na kubwa. Au huenda hajui njia nzuri ya ulinganizi au kwa sababu nyinginezo. Hivyo aangalie na ajipime nafsi yake na amche Allaah. Hakika hafanikiwi isipokuwa kwa sababu ya dhambi katika dhambi zake, jambo ambalo mara nyingi ndilo hutokea. Huenda pia akawa hasikilizwi hata kama ni mtengemavu zaidi ya watu, lakini aihesabu na kuiangalia nafsi yake. Akiuona upungufu au kosa alitibu, na asipoona kitu basi ni vyema na hilo halitomdhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikaa Makkah muda mrefu – miaka kumi na tatu – lakini waliomkubali walikuwa wachache tu. Hata hivyo hilo halikumdhuru. Kama mlivyosikia katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas ambaye amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Nilionyeshwa ummah na nikamwona Mtume akiwa na kundi dogo.”
Imekuja kaktika riwaya ya Muslim:
”… kundi dogo la watatu, wanne au watano. Mtume mwingine akiwa na mtu mmoja au wawili. Mtume mwingine bila mtu yeyote.”
Baadhi ya Manabii hakuna mtu hata mmoja aliyemtii kabisa. Hawakukubaliwa kutoka kwake. Bali walimuua. Atakuja siku ya Qiyaamah peke yake akiwa hana mtu yeyote katika ummah wake aliyemfuata. Lakini hilo halitomdhuru. Hata hivyo huyu atakuwa ametekeleza wajibu wake.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29416/%D9%85%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%88%D8%AC%D9%8A%D9%87%C2%A0%D9%84%D9%85%D9%86-%D9%8A%D9%86%D8%B5%D8%AD-%D9%84%D9%84%D9%86%D8%A7%D8%B3-%D8%AF%D9%88%D9%86-%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D8%AC%D8%A7%D8%A8%D8%A9
Imechapishwa: 10/08/2025
https://firqatunnajia.com/zipi-nasaha-zako-kwa-ambaye-hauitikiwi-ulinganizii-wake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket