Swali 9407: Nimewaona baadhi ya watu wakitumia vitu vinavyobadilisha rangi ya nywele, ni mamoja iwe vinaifanya iwe nyeusi au nyekundu. Pia nimewaona wakitumia vitu vingine vinavyofanya nywele zilizojisokota kuwa laini. Je, kuna chochote katika mambo hayo kinachojuzu? Je, vijana na wazee wana hukumu sawa katika jambo hilo?
Jibu: Hapana neno kubadilisha rangi ya nywele kwa rangi isiyo nyeusi. Vilevile kutumia vitu vya kulainisha nywele zilizojisokota. Hukumu kwa vijana na wazee katika jambo hilo ni sawa, ikiwa hakuna madhara na kitu hicho ni twahara na kinaruhusiwa. Ama kubadilisha kwa rangi nyeusi kabisa, haijuzu kwa wanaume na wanawake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Badilisheni mvi hii na jiepusheni na rangi nyeusi.”[1]
[1] Ahmad (03/338), Muslim (06/155) na Abu Daawuud (4204).
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/168)
- Imechapishwa: 23/10/2026
Swali 9407: Nimewaona baadhi ya watu wakitumia vitu vinavyobadilisha rangi ya nywele, ni mamoja iwe vinaifanya iwe nyeusi au nyekundu. Pia nimewaona wakitumia vitu vingine vinavyofanya nywele zilizojisokota kuwa laini. Je, kuna chochote katika mambo hayo kinachojuzu? Je, vijana na wazee wana hukumu sawa katika jambo hilo?
Jibu: Hapana neno kubadilisha rangi ya nywele kwa rangi isiyo nyeusi. Vilevile kutumia vitu vya kulainisha nywele zilizojisokota. Hukumu kwa vijana na wazee katika jambo hilo ni sawa, ikiwa hakuna madhara na kitu hicho ni twahara na kinaruhusiwa. Ama kubadilisha kwa rangi nyeusi kabisa, haijuzu kwa wanaume na wanawake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Badilisheni mvi hii na jiepusheni na rangi nyeusi.”[1]
[1] Ahmad (03/338), Muslim (06/155) na Abu Daawuud (4204).
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/168)
Imechapishwa: 23/10/2026
https://firqatunnajia.com/zipake-ndevu-rangi-isiyo-nyeusi/