Swali: Ni ipi hukumu ya kula vyakula ambavyo vinavyotengenezwa katika sherehe ya mwaka wa kuzaliwa?
Jibu: Hapa kunahitaji upambanuzi. Ikiwa chakula hichi ni katika vile vyakula vinavyopikwa kwa ajili ya mnasaba huu peke yake, kwa mfano zile tamtam zinazoitwa ´tamzam za mwaka wa kuzaliwa`, haijuzu kuzitumia. Lakini ikiwa chakula hicho hakipikwi katika mnasaba peke hake, bali kinapikwa wakat wowote, lakini kinaliwa katika mnasaba huu hakuna neno kukila. Lakini ukipewa nacho zawadi unatakiwa ukirudishe. Hukirudishi chenyewe kama chenyewe. Lakini unakirudisha kwa sababu ya kukaripia sherehe iliyokatazwa. Kwa mfano chakula kwa ajili ya siku ya mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), chakula kwa ajili ya sherehe ya kuzaliwa au chakula cha krismasi. Ukiletewa chakula wakati kama huo unatakiwa kukirudisha. Haijalishi kitu hata kama wao wanakula chakula hicho kimazowea. Lakini kama kitaliwa katika mnasaba huu na wewe ukapewa zawadi nacho unatakiwa kukirudisha. Kwa nini? Kwa sababu ya kukemea sherehe zao. Lakini inafaa kukitumia? Ndio, inafaa kwa sharti isiwe ni chenye kutengenezwa katika mnasaba huu peke yake.
- Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=w_8gknDhre8
- Imechapishwa: 12/04/2020
Swali: Ni ipi hukumu ya kula vyakula ambavyo vinavyotengenezwa katika sherehe ya mwaka wa kuzaliwa?
Jibu: Hapa kunahitaji upambanuzi. Ikiwa chakula hichi ni katika vile vyakula vinavyopikwa kwa ajili ya mnasaba huu peke yake, kwa mfano zile tamtam zinazoitwa ´tamzam za mwaka wa kuzaliwa`, haijuzu kuzitumia. Lakini ikiwa chakula hicho hakipikwi katika mnasaba peke hake, bali kinapikwa wakat wowote, lakini kinaliwa katika mnasaba huu hakuna neno kukila. Lakini ukipewa nacho zawadi unatakiwa ukirudishe. Hukirudishi chenyewe kama chenyewe. Lakini unakirudisha kwa sababu ya kukaripia sherehe iliyokatazwa. Kwa mfano chakula kwa ajili ya siku ya mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), chakula kwa ajili ya sherehe ya kuzaliwa au chakula cha krismasi. Ukiletewa chakula wakati kama huo unatakiwa kukirudisha. Haijalishi kitu hata kama wao wanakula chakula hicho kimazowea. Lakini kama kitaliwa katika mnasaba huu na wewe ukapewa zawadi nacho unatakiwa kukirudisha. Kwa nini? Kwa sababu ya kukemea sherehe zao. Lakini inafaa kukitumia? Ndio, inafaa kwa sharti isiwe ni chenye kutengenezwa katika mnasaba huu peke yake.
Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=w_8gknDhre8
Imechapishwa: 12/04/2020
https://firqatunnajia.com/zawadi-ya-chakula-unachopewa-katika-minasaba-ya-kizushi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)