Zakaah ya biashara zenye kujibadili mara kwa mara kabla ya kutimiza mwaka

Swali: Mara nyingi wanawake hawajui dhahabu inayowajibika kuitolea zakaah kwa kuwa anaifanyia biashara ya kununua na kuiuza na kuibadili. Katika hali hii dhahabu mara nyingi haibaki kwa mwaka na haifikishi mwaka. Ni ipi hukumu kwa hili?

Jibu: Ikiwa dhahabu hii mwanamke anainunua na kuiuza, midhali anaiuza na inafikisha mwaka ina zakaah hata kama anaiuza na kuinunulia. Katika hali hii anachotakiwa kuzingatia ni ule mwaka wa kwanza. Kadhalika biashara zingine zote za mzunguko haishurutishwi kufikisha mwaka. Kwa mfano amenunua ardhi katika mwezi wa Muharram, zakaah inakuwa wajibu katika mwezi Muharram wa kufuata. Ardhi hii nikawa nimeiuza katika Dhul-Hijjah na nikanunua ardhi nyingine na mwezi wa Muharram ukaingia, je, nitolee zakaah ile ardhi nyingine au niseme kuwa ardhi ile haikufikisha mwaka? Jibu ni kuwa napaswa kutolea zakaah ile ardhi ya kwanza hata kama niliimiliki miezi kumi na moja tu. Biashara ya mzunguko haishurutishi kutimia kwa mwaka, kila wakati inabadilika utafikiri ni bidhaa moja.

Mwanamke huyu alie na dhahabu ambayo anaiuza na kununua kwa pesa za dhahabu hiyo na vilevile anaitumia kwa kuivaa, tunasema kuwa huyu haishurutishwi kile kitu cha mwisho kufikisha mwaka. Kinachozingatiwa ni ule mwaka wa kwanza. Kwa mfano ameiuza mara ya kwanza na zakaah yake itaeneza mwaka katika Ramadhaan na ndani ya muda huu anauza dhahabu hii na kununua nyingine, ilipofika Sha´abaan akanunua dhahabu nyingine mpya, tunasema itapofika Ramadhaan tolea zakaah dhahabu hii hata kama kutakuwa hakukubaki isipokuwa mwezi mmoja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 02
  • Imechapishwa: 23/09/2020