Swali: Mimi ni katika familia yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nimeambiwa kuwa haifai kwangu kula swadaqah na mali ya wapita njia. Je, hilo ni sahihi? Je, maji yaliyoekwa kwa kunywa misikitini nayo yanaingia humo?

Jibu: Hapana, hayo hayaingii. Kilichokatazwa ni zakaah tu. Ama kunywa maji misikitini, swadaqah ya kujitolea au mapato ya waqf, hapana vibaya. Kilichokatazwa kwa watu wa familia yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni zakaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika haistahiki kwa watu wa familia yake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hapana hapana vyengine hiyo ni katika uchafu wa watu.”

Kwa maana ya zakaah tu. Watu wa familia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kile kizazi cha Haashim peke yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30942/حكم-الزكاة-والصدقة-لمن-كان-من-ال-البيت
  • Imechapishwa: 14/09/2025