Zakaah kwa watoto walio chini ya uangalizi wa mtu

Swali: Swadaqah na zakaah vinajuzu kutolewa kwa mayatima walio chini ya usimamizi wangu kwa kuwa mimi ni mume wa mama yao hali ya kuwa mimi si mlezi wao?

Jibu: Ikiwa wao ni mafakiri, inajuzu kuwapa kutoka katika zakaah. Unaweza kuwanunulia mavazi kwa ajili yao. Ama chakula, basi wanakula pamoja na chakula chako wewe na utapata ujira, in shaa Allaah. Lakini ikiwa kuna haja ya mavazi, basi kuwatosheleza kwa kutumia zakaah hakuna ubaya.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1426/حكم-صرف-الزكاة-لابناء-الزوجة-الذين-في-كفالة-الزوج
  • Imechapishwa: 19/12/2025