Swali: Je, anapewa kutoka katika zakaah au kutoka katika matumizi aliyepoteza biashara yake na kufilisika?

Jibu: Huyu na huyu, ikiwa ni maskini basi anapewa kutoka katika swadaqah na kutoka katika zakaah.

Swali: Je, watu waonywe wasifanye muamala na aliyefilisika?

Jibu: Hapana, si lazima.

Swali: Anawadanganya watu kwa kula haki zao na hili limeenea sasa hivi? Je, haonywi kuhusu yeye na kufanya hivo si kusengenya?

Jibu: Hili linahitaji kuangaliwa vyema. Ama kuhusu haki yake yeye aliyedhulumiwa, ana haki ya kumshitakia na kusema “Amenidhulumu, amenibatilishia haki yangu” kwa sababu yeye ni mwenye kudhulumiwa. Lakini suala la kuwajulisha watu kwamba yeye amefilisika, hili linahitaji kuangaliwa vyema, kwa kuwa huenda akawa amelazimika kununua mahitaji yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25401/هل-تجوز-الزكاة-للمفلس-وهل-يحذر-الناس-منه
  • Imechapishwa: 09/03/2025