Yuko na maji ya kuoga janaba lakini hana bafu

Swali: Nilikuwa safarini nikaota ndoto na nikatokwa na manii. Kulikuwa na maji ambayo ningeweza kuoga janaba, lakini hakukuwa na sehemu ya kuogea. Nifanye nini kuhusu swalah?

Jibu: Ni lazima uoge ikiwa manii yatatoka kwako kwa sababu ya kuota ndoto. Kutokuwepo kwa sehemu maalum ya kuogea si udhuru wa kuacha kuoga. Unaweza kumuomba mmoja wa wenzako akusitiri kwa shuka, kisha ukaoga.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/304)
  • Imechapishwa: 14/11/2026