Swali: Wakati mwingine ninaota usiku mambo yanayonifanya niwe na janaba katika usingizi wangu. Ninapoamka – na mnajua kwamba siku hizi baridi ni kali – huenda shuleni bila kupata fursa ya kuoga. Nasoma Qur-aan darasani na naswali Fajr na Dhuhr hali ya kuwa nina janaba. Je, nina jambo lolote juu ya nililolitaja?

Jibu: Ni lazima uoge baada ya kuota ndoto ikiwa umeona manii na una kitu cha kupasha maji joto. Aidha ni lazima urudie swalah ulizoswali bila kuoga. Haijuzu kwako kugusa msahafu ukiwa na janaba, wala kusoma Qur-aan kabla ya kuoga.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/305)
  • Imechapishwa: 14/11/2026