Aliyemwaga baada ya ndoto ya jimaa anaoga kama aliyemjamii mke wake?

Swali: Je, mtu aliyeota ndoto ya kujamii analazimika kuoga kama kuoga janaba? Ni namna gani ya kuoga janaba?

Jibu: Ni lazima kwake kuoga janaba ikiwa manii yamemtoka kwa sababu ya kuota ndoto. Kuhusu namna ya kuoga janaba, inamtosheleza kueneza maji katika mwili wake wote. Lakini bora ni kuondoa uchafu ulioko mwilini mwake, kisha atawadhe kama anavyotawadha kwa ajili ya swalah, kisha apitishe vidole katika nywele za kichwa chake, halafu amimine mafungu matatu ya maji juu ya kichwa chake, kisha aeneze maji katika mwili wake wote.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/306)
  • Imechapishwa: 14/11/2026