Yuko mji mwingine mbali na wakeze kwa muda wa mwaka na nusu

Swali: Mimi nafanya kazi katika shirika moja liliopo nchini Sudan. Niko mbali na mke wangu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu sasa. Sababu ya kuwa kwangu mbali ni kutafuta riziki yangu mwenyewe na ya watoto wangu. Nina wake wawili na watoto kumi. Hii ndio sababu ya mimi kuwa mbali na wake zangu wawili. Je, ni mwenye kusemwa vibaya kwa kuwa kwangu mbali na wake zangu? Ni vipi nitayatatua?

Jibu: Ikiwa wakezo ni wenye kuridhia hilo basi si mwenye kulaumiwa kabisa. Wakiwa hawako radhi basi kuliendea kwako jambo la lazima ambalo litapelekea kuwa mbali nao hakuna ubaya. Lakini ni lazima hilo liwe limefungamana na desturi. Kwa msemo mwingine usiwe mbali kwa njia ya kukata ambayo watu wanaichukulia kama kumhama mtu. Ni lazima kwako kwenda kwao mara kwa mara na wakati mwingine unaenda kutafuta riziki ili utekeleze majukumu yako kwa pande zote mbili; jukumu la matangamano kati ya mume na mke na jukumu kuwahudumikia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (07) http://binothaimeen.net/content/6714
  • Imechapishwa: 11/11/2020