Wudhuu´ wa mwenye rangi ya kucha

Swali: Tumewasikia baadhi ya wanazuoni wakisema kwamba inajuzu mwanamke kutawadha bila kuondoa rangi ya kucha. Unasemaje kuhusu jambo hili?

Jibu: Ikiwa rangi hiyo ina tabaka juu ya kucha, basi wudhuu´ wake hautosihi bila kuiondoa kabla ya kutawadha. Ama ikiwa haina tabaka juu ya kucha, basi wudhuu´ wake ni sahihi, kama ilivyo kwa hina.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/218-219)
  • Imechapishwa: 06/11/2026