Wudhuu´ wa aliyetawadha akiwa uchi

Swali: Nilipomaliza kuoga kwa ajili ya kujitwaharisha nilitawadha kisha nikatoka bafuni na kuvaa nguo zangu. Je, kitendo changu ni sahihi? Nikimaanisha kwamba kufunika uchi ni sharti katika kusihi wudhuu´?

Jibu: Wudhuu´ ni sahihi. Kufunika uchi si sharti katika kusihi wudhuu´.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/101)
  • Imechapishwa: 19/02/2026