Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أَبي رُقَيَّةَ تَمِيم بن أوس الداريِّ رضي الله عنه: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (الدِّينُ النَّصِيحةُ) قلنا: لِمَنْ؟ قَالَ: (لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلأئِمَّةِ المُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ))

181- Abu Ruqayyah Tamiym bin Aws ad-Daariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dini ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani?” Akasema: “Kwa Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na waislamu wa kawaida.”[1]

Miongoni mwa nasaha mtu wivu wake uwe kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) pale kunapoendewa yale aliyoharamisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa namna hii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa maishani halipizi [adhabu au kisasi] kwa ajili ya nafsi yake. Vovyote watu watasema juu yake halipizi juu ya nafsi yake. Lakini pale tu yanapoendewa yale aliyoharamisha Allaah, basi anakuwa mkali kabisa kwa kumlipiza yule mtendaji.

Hivyo mtu awe na wivu juu ya Mola Wake. Asimwache yeyote akamtukana au kumsema vibaya au kumfanyia mzaha Allaah. Akifanya hivo awe na wivu kwa ajili ya Allaah kwa hilo na amkemee hata ikibidi kwenda kumshtaki kwa mtawala afanye hivo. Kwa sababu hii ni miongoni mwa nasaha kwa Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Muslim

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/384-385)
  • Imechapishwa: 27/07/2025