Wavivu wanapoiswali na wakati wa kwenda msikitini

Swali: Tafsiri ya Aayah isemayo:

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا

“Hakika wanafiki wanafikiri wanamhadaa Allaah na hali Yeye ndiye Mwenye kuwahadaa na wanaposimama kuswali basi husimama kwa uvivu, wakijionyesha kwa watu na wala hawamtaji Allaah isipokuwa kidogo tu.” (04:142)

Je, makusudio ni kujichelewesha kuhudhuria msikitini?

Jibu: Yote mawili. Uvivu wakati wa kuswali, kukiwemo swalah inayopendeza, pia uvivu wakati wa kwenda kwao misikitini. Kwa msemo mwingine hawana uchangamfu wenye kutosheleza kutokana na udhaifu wa imani. Kwa ajili hiyo ndio maana wana uvivu wakati wa kuiswali katika mkusanyiko na vilevile ni wavivu wakati wa kuiswali nyumbani. Hatimaye hata nyumbani wanaiacha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21910/معنى-واذا-قاموا-الى-الصلاة-قاموا-كسالى
  • Imechapishwa: 01/10/2022