Swali 715: Vipi kuhusu vifaa vya kuua wadudu vinavyowapiga kwa mshtuko wa umeme?

Jibu: Hapana, bali wauliwe kwa dawa nyingine za kuulia wadudu zisizo na moto[1].

[1] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn amesema katika kitabu chake kuhusu kuua kwa njia ya umeme: “Si kuua kwa moto. Dalili ya hili ni kwamba mwathiriwa wala nguo zao haziunguzwi. Bali wanauawa kwa kupigwa na umeme (mshituko wa umeme), ambao huganda damu na kusababisha kifo cha kudumu.” (Majmuu’-ul-Fatawa” (16/25))

Kuna nguvu katika maneno yake, lakini kuna upanuzi katika matumizi yake – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 250
  • Imechapishwa: 05/07/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´