Kutoka kwa mtoto… kwenda kwa baba muheshimiwa Shaykh Muhammad bin Swaalih bin al-´Uthaymiyn
السلام عليكم و رحمة الله و بركاته
Naomba mlindwe daima. Nasi – himdi zote njema anastahiki Allaah – tuko kama mnavopenda. Tunakupongezeni kwa mwezi huu uliobarikiwa. Tunamuomba Allaah atujaalie kuwa miongoni mwa wenye kuufunga na kusimama swalah ya usiku kwa njia kamilifu zaidi.
Je, mwanamke mwenye mimba na mwenye kunyonyesha wakichelea juu ya watoto wao watalipa masiku yao waliyokula au watalipa pamoja na kulisha chakula kuwapa masikini? Nipe fatwa, Allaah akulipe Pepo kwa rehema na ukarimu Wake.
بسم الله الرحمن الرحيم
و عليكم السلام و رحمة الله و بركاته
Tunakushukuruni kwa pongezi za mwezi wa Ramadhaan. Tunataraji Allaah kutuwafikisha sote juu ya yale anayoyapenda na kuyaridhia na atukubalie sote.
Kuhusu uliyoyataja juu ya mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha ambao wanakula kwa sababu ya kukhofia juu ya watoto wao, madhehebu yanaona mosi kuwa wanapaswa kuyalipa masiku yao, pili mlezi wa mtoto huyo pia atalisha chakula kumpa masikini kwa kila moja aliyoacha kufunga. Lakini nahisi kitu moyoni mwangu juu ya hilo. Naegemea zaidi juu ya maoni yanayosema kuwa hakuna kinachowalazimu isipokuwa kuyalipa tu masiku hayo. Mlezi wa mtoto halazimiki kulisha chakula, kwa sababu hakuna dalili tosha yenye nguvu juu ya hilo. Hilo ndilo la wajibu. Allaah akuhifadhini. Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yenu na juu ya yale mnaowapenda.
Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn
1397-09-07
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/159-160)
- Imechapishwa: 31/03/2026
Kutoka kwa mtoto… kwenda kwa baba muheshimiwa Shaykh Muhammad bin Swaalih bin al-´Uthaymiyn
السلام عليكم و رحمة الله و بركاته
Naomba mlindwe daima. Nasi – himdi zote njema anastahiki Allaah – tuko kama mnavopenda. Tunakupongezeni kwa mwezi huu uliobarikiwa. Tunamuomba Allaah atujaalie kuwa miongoni mwa wenye kuufunga na kusimama swalah ya usiku kwa njia kamilifu zaidi.
Je, mwanamke mwenye mimba na mwenye kunyonyesha wakichelea juu ya watoto wao watalipa masiku yao waliyokula au watalipa pamoja na kulisha chakula kuwapa masikini? Nipe fatwa, Allaah akulipe Pepo kwa rehema na ukarimu Wake.
بسم الله الرحمن الرحيم
و عليكم السلام و رحمة الله و بركاته
Tunakushukuruni kwa pongezi za mwezi wa Ramadhaan. Tunataraji Allaah kutuwafikisha sote juu ya yale anayoyapenda na kuyaridhia na atukubalie sote.
Kuhusu uliyoyataja juu ya mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha ambao wanakula kwa sababu ya kukhofia juu ya watoto wao, madhehebu yanaona mosi kuwa wanapaswa kuyalipa masiku yao, pili mlezi wa mtoto huyo pia atalisha chakula kumpa masikini kwa kila moja aliyoacha kufunga. Lakini nahisi kitu moyoni mwangu juu ya hilo. Naegemea zaidi juu ya maoni yanayosema kuwa hakuna kinachowalazimu isipokuwa kuyalipa tu masiku hayo. Mlezi wa mtoto halazimiki kulisha chakula, kwa sababu hakuna dalili tosha yenye nguvu juu ya hilo. Hilo ndilo la wajibu. Allaah akuhifadhini. Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yenu na juu ya yale mnaowapenda.
Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn
1397-09-07
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/159-160)
Imechapishwa: 31/03/2026
https://firqatunnajia.com/watayalipa-tu-masiku-yao/