Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah kuhusu madereva wa kigeni wanaotoka na wanawake peke yao nje ya nyumba zao, kuwapeleka sokoni na bustanini na wakati mwingine nje ya mji kwa kisingizio cha kuwa yeye ni dereva wao?
Jibu: Dereva, ikiwa sio Mahram wa mwanamke, haijuzu kukaa naye chemba. Bali ni lazima wawe watatu au zaidi. Ikiwa anataka kwenda sokoni au shuleni, lazima wawe watatu. Asiondoke na msichana kwenda shule peke yake, wala na mwanamke kwenda sokoni peke yake. Ni lazima awepo mtu wa tatu; awe kaka yake, mama yake, mke wa dereva, mwanaume mwingine au mwanamke mwingine ambaye kwa kuwepo kwake itazuilika faragha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanaume hakai faragha na mwanamke isipokuwa shaytwaan huwa ni watatu wao.”
Hivyo haijuzu dereva kukaa naye chemba, siyo kwenda naye shuleni wala sehemu nyingine yoyote. Bali lazima wawepo wengine ambao kwa kuwepo kwao itandole ile faragha, kutakuwa na utulivu na kuondoka shaka.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30107/ما-حكم-الخلوة-بساىق-الاسرة-الاجنبي
- Imechapishwa: 11/09/2025
Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah kuhusu madereva wa kigeni wanaotoka na wanawake peke yao nje ya nyumba zao, kuwapeleka sokoni na bustanini na wakati mwingine nje ya mji kwa kisingizio cha kuwa yeye ni dereva wao?
Jibu: Dereva, ikiwa sio Mahram wa mwanamke, haijuzu kukaa naye chemba. Bali ni lazima wawe watatu au zaidi. Ikiwa anataka kwenda sokoni au shuleni, lazima wawe watatu. Asiondoke na msichana kwenda shule peke yake, wala na mwanamke kwenda sokoni peke yake. Ni lazima awepo mtu wa tatu; awe kaka yake, mama yake, mke wa dereva, mwanaume mwingine au mwanamke mwingine ambaye kwa kuwepo kwake itazuilika faragha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanaume hakai faragha na mwanamke isipokuwa shaytwaan huwa ni watatu wao.”
Hivyo haijuzu dereva kukaa naye chemba, siyo kwenda naye shuleni wala sehemu nyingine yoyote. Bali lazima wawepo wengine ambao kwa kuwepo kwao itandole ile faragha, kutakuwa na utulivu na kuondoka shaka.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30107/ما-حكم-الخلوة-بساىق-الاسرة-الاجنبي
Imechapishwa: 11/09/2025
https://firqatunnajia.com/watatu-wa-dereva-na-mwanamke-ni-shaytwaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket