Swali: Je, wasia hutangulizwa kabla ya deni?

Jibu: Hapana, deni hutangulizwa kabla ya kila kitu. Allaah amesema:

مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ

”… baada ya kutoa wasia aliousia maiti au kulipa deni.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alihukumu kwamba deni linapaswa kulipwa kabla ya wasia.

[1] 04:11

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25387/هل-يجوز-تقديم-الوصية-على-الدين
  • Imechapishwa: 08/03/2025