Swali: Dada mmoja anauliza na kusema ni ipi hukumu ya kuiga mavazi na mitindo ya nguo za Magharibi kupitia majarida ya mitindo ya mavazi?

Jibu: Haijuzu kwa wanawake waislamu wala wanaume waislamu kuiga Magharibi au Mashariki katika nguo zao mahsusi ambazo si katika ada ya waislamu. Hii ni kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) ametukataza kujifananisha na kuiga maadui zetu. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah Naye akazisahaulisha nafsi zao – hao ndio mafasiki.”[1]

كَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوا أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا فَاسْتَمْتَعُوا بِخَلَاقِهِمْ فَاسْتَمْتَعْتُم بِخَلَاقِكُمْ كَمَا اسْتَمْتَعَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَاقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَالَّذِي خَاضُوا ۚ أُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ

”Ni kama wale wa kabla yenu walikuwa wana nguvu zaidi kuliko nyinyi na wana mali na watoto wengi zaidi. Basi waliburudika kwa fungu lao nanyi burudikeni kwa fungu lenu kama walivyoburudika kwa fungu lao wale wa kabla yenu na mkazama katika batili na ukanushaji kama wao walivyotumbukia. Hao yameporomoka matendo yao duniani na Aakhirah – na hao ndio waliokhasirika.”[2]

Amewasema vibaya na kuwasimanga kwa kuwaiga maadui.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote mwenye kuwaiga watu basi yeye ni katika wao.”

“Punguzeni masharubu na achieni ndevu, jitofautisheni na washirikina.”

“Kateni masharubu na fugeni ndevu, jitofautisheni na waabudia moto.”

Zipo Hadiyth nyingi.

Kwa hiyo ni wajibu kwa wanaume wa Kiislamu na wanawake wa Kiislamu kutokujifananisha na maadui wa Allaah katika nguo zao maalum na wajiepushe na hayo popote walipo, kutokana na dalili zilizotangulia.

[1] 59:19

[2] 09:69

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30012/ما-حكم-تقليد-الكفار-في-ازياىهم-وملابسهم
  • Imechapishwa: 27/08/2025