Swali: Tunaomba nasaha kutoka kwenu kuhusu yanayofanyika katika mji wa Jiyzan, ambapo panapokuwa na hafla ya ndoa au kutahiriwa, wanaume huingia wakipiga ngoma na hupiga ngoma katikati ya wanawake na huku wanawake wakiwatupia pesa, nao wanacheza bila haya mbele ya Allaah?
Jibu: Hili tayari limeelezwa kwao na wameandikiwa kuhusu jambo hili. Walinganiaji walioko huko wamepewa jukumu la kulibainisha jambo hili. Tunamuomba Allaah awaongoze wote.
Watu wengi husikia nasaha lakini hawazingatii na huona desturi waliyoizoea kuwa ni lazima, kisha wanaitanguliza juu ya yale aliyosema Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mitume na walinganiaji hawakupingwa isipokuwa kwa sababu ya desturi, desturi zinazopingana na Shari´ah. Desturi za kabla ya kuja Uislamu ndizo zilizokuwa sababu ya kupingwa kwa Mitume na walinganiaji.
Hivyo ni wajibu kwa muislamu kujiepusha na desturi mbaya inayopingana na Shari´ah na asidanganywe na yale waliokuwa nayo mababu zake ikiwa ni batili. Desturi hazitolewi hoja, bali hupimwa kwa dalili za Shari´ah. Zikiwa sahihi, basi zinachukuliwa. Vinginevyo lazima ziachwe, hata kama ni desturi za wazazi na mababu. Haifai kwa mwenye akili kuwa kama walivyosema makafiri wajinga:
إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ
“Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini na hakika sisi ni wenye kufuata nyao zao.”[1]
Hii ni hoja ya makafiri waliyotumia kupinga Mitume, nayo ni hoja batili isiyokubalika. Haifai kwa muislamu kuitumia. Bali ni wajibu kupeleka mambo yote yenye utata kwa dalili za Shari´ah na kuwauliza wanazuoni. Asiseme:
“Hii ni ada ya baba yangu, babu yangu au watu wa mji wangu.”
na akatosheka nayo, hata kama inapingana na Shari´ah.
Swali: Nyinyi mnasema mnawaandikia watu wa kawaida, lakini nilipokwenda kwa familia yangu niliwakuta bado wako katika hali ileile, hata zaidi?
Jibu: Hata hivyo barua zimewafikia mara nyingi kuhusu hilo na walinganiaji wamewasomea. Lakini desturi – kama ilivyosemwa – huwa zinawatawala watu. Ni wachache sana wanaoziacha. Tunamuomba Allaah atupe usalama na atuongoze sisi na wao.
[1] 43:23
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3168/حكم-دخول-الرجال-بين-النساء-في-مناسبات-الزواج
- Imechapishwa: 02/11/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3168/حكم-دخول-الرجال-بين-النساء-في-مناسبات-الزواج
Imechapishwa: 02/11/2026
https://firqatunnajia.com/wanaume-kuchanganyika-na-wanawake-katika-minasaba-ya-ndoa/