Ni lazima tufuate mfumo au mwenendo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kuchagua watawala na mahakimu. Basi haifai kupewa nyadhifa hizi kwa yule aliyeziomba, anayezipupia au kwa mfano yule anayejiweka mwenyewe kama mgombea kwa njia ya uchaguzi, kwani hiyo ni ishara ya kupenda madaraka. Bali anachaguliwa kwa ajili ya kazi hizi wale watu wenye elimu, kujiepusha nayo na wenye kumcha Allaah.

Kisha tunapaswa kunufaika na mwenendo huu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika malezi. Basi haifai kabisa kuwalea vijana juu ya kupenda uongozi, utawala, ukuu na cheo. Kwa kuwa tukiwalea juu ya kupenda mambo haya, basi tutakuwa tumeenda kinyume na uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na tumewaingiza vijana katika maangamizi. Je, kuna mafanikio tunayoyatarajia ulimwenguni na Aakhirah ikiwa tutaenda kinyume na mwenendo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

وَيَقُولُونَ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالرَّسُولِ وَأَطَعْنَا ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ وَإِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم مُّعْرِضُونَ

”Wanasema: “Tumemwamini Allaah na Mtume na tumetii” kisha hugeuka kundi miongoni mwao baada ya hayo na wala hao si wenye kuamini. Wanapoitwa kwa Allaah na Mtume Wake ili awahukumu baina yao mara hapo kundi miongoni mwao wanakengeuka.”[1]

[1] 24:47-48

  • Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj-ul-Anbiyaa´ fiyd-Da´wah ilaa Allaah fiyhi al-Hikmah wal-´Aql, uk. 124
  • Imechapishwa: 19/02/2017