Swali: Mnasemaje kuhusu mtu aliyesema kwamba hakuna tofauti kati ya Sunniy na Shiy´ah, bali wote ni waislamu. Mtu huyo ni Muftiy katika moja ya nchi za Kiislamu na amefanyiwa mahojiano katika mojawapo ya majarida mwezi uliopita. Aidha anasema kuwa ni haramu kwetu kusema huyu ni Sunniy na huyu ni Shiy´ah. Je, maneno haya hayana tatizo au mnaonaje?
Jibu: Maneno haya yana ujumla wenye kosa. Hakika Shiy´ah ni makundi, si kundi moja. Shiy´ah ni makundi mengi. ash-Shahrastaaniy ametaja kwamba ni makundi ishirini na mawili. Wao wanatofautiana. Miongoni mwao wapo ambao Bid´ah zao zinamfanya mtu kuwa kafiri na miongoni mwao wapo ambao Bid´ah zao hazimfanyi kuwa kafiri, pamoja na kwamba kwa ujumla wao ni wat wa Bid´ah. Wa chini yao kabisa ni yule anayemfanya ´Aliy kuwa bora zaidi kuliko Abu Bakr as-Swiddiyq na ´Umar, huyu amekosea na amewapingana na Maswahabah. Lakini khatari zaidi miongoni mwao ni Raafidhwah, wafuasi wa Khumayniy. Hawa ndio khatari zaidi. Vivyo hivyo Nuswayriyyah, wafuasi wa Haafidhw al-Asad na kundi lake huko Syria. Baatwiniyyah walioko Syria, walioko Iran na walioko India ambao ni al-Ismaa´iyliyyah. Makundi haya matatu ndiyo mabaya na khatari zaidi, nao ni makafiri. Hawa ni makafiri kwa sababu – tunajilinda kwa Allaah – wanaficha uovu kwa waislamu, wanaona waislamu ni khatari zaidi kwao kuliko makafiri na wanawachukia waislamu zaidi kuliko wanavyowachukia makafiri. Wanaona kuwa Ahl-us-Sunnah ni halali damu zao na mali zao, hata kama wanajipendekeza katika baadhi ya maeneo. Wanaamini kwamba maimamu wao wanajua ghaibu, kwamba wao hawakosei na wanawaabudu badala ya Allaah kwa kuwaomba msaada, kuwachinjia na kuwawekea nadhiri. Hii ndiyo hali yao kwa maimamu wao. Raafidhwah ambao ni kundi la Ithnaa ´Ashariyyah, wanaitwa pia Ja´fariyyah na leo wanaitwa Khumayniyyah. Hawa wanalingania batili. Ni miongoni mwa makundi mabaya zaidi. Vivyo hivyo Nuswayriyyah ni katika makundi mabaya zaidi na pia al-Ismaa´iyliyyah. Hawa ni Baatwiniyyah. Wanaona uongozi wa as-Swiddiyq, ´Umar na ´Uthmaan ni batili. Aidha wanaona Maswahabah kuwa makafiri waliotoka katika Uislamu isipokuwa wachache kama ´Aliy, al-Hasan, al-Husayn, ´Ammaar bin Yaasir na wawili au watatu au wanne wengine wanaodai kuwa walimuunga mkono ´Aliy tu. Ama Maswahabah wengine kwao ni waasi waliotoka katika Uislamu, walimdhulumu ´Aliy na mengineyo wanayosema.
Pamoja na hayo wanapetuka mipaka kwa watu wa familia yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanadai kuwa wanajua ghaibu na kwamba uongozi ni wao tu na kwamba tawala zote baada ya ´Aliy na kabla yake ni batili na kwamba hakuna uongozi wa haki isipokuwa wa ´Aliy na al-Husayn tu. Ama tawala zote tangu zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka leo kwao ni batili. Tunamuomba Allaah atupe salama.
Kwa kumalizia Shiy´ah ni makundi, si kundi moja. Miongoni mwao wapo Zaydiyyah wanaojulikana Yemen. Hawa wana ´Aqiydah ya kumfanya ´Aliy kuwa ndiye bora, lakini si makafiri isipokuwa wale miongoni mwao wanaoabudu masanamu au wanachupa mipaka kwa watu wa familia yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaomba badala ya Allaah. Ama kile kitendo cha kumfanya ´Aliy kuwa bora zaidi kuliko as-Swiddiyq na ´Umar si kufru, bali ni Bid´ah na kosa. Ni wajibu kumfanya as-Swiddiyq kuwa ndiye bora zaidi, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan kabla ya ´Aliy. ´Aliy ni wa nne (Radhiya Allaahu ´anh). Hii ndiyo haki iliyokubaliwa na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Anayemfadhilisha ´Aliy juu yao amekosea, lakini si kafiri. Makafiri miongoni mwao ni Raafidhwah, Nuswayriyyah na Ismaa´iyliyyah ambao wanachupa mipaka kwa watu wa familia yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanawaabudu badala ya Allaah, wanaamini kuwa maimamu wao wanajua ghaibu na mengineyo wanayoyasema.
Kwa hiyo lazima kuangalia ´Aqiydah zao kwa undani, wala haisemwi kuwa Shiy´ah wote ni makafiri, hapana. Bali ni suala linahitaji upambanuzi na ni makundi mengi.
Swali: Hajj yao kwenda katika Nyumba ya Allaah Tukufu inakuwaje kwa kuzingatia ´Aqiydah hii?
Jibu: Lazima jambo lao liangaliwe baadaye. Tunamuomba Allaah awafanikishe watawala kwa kila kheri na awasaidie.
Swali: Kwa nini wanakasirika kuitwa majina ya Abu Bakr, ´Uthmaan, ´Aaishah, Hafswah na Umm Habiybah?
Jibu: Ni jambo linalojulikana. Wanaona as-Swiddiyq ni kafiri, ´Umar ni kafiri, ´Uthmaan ni kafiri na wanadai walimdhulumu ´Aliy, wanamtuhumu ´Aaishah na mengineyo katika ´Aqiydah zao batili.
Kwa kumalizia ´Aqiydah ya anayesema hakuna tofauti kati ya Shiy´ah na Sunniy ni batili yenye kosa. Shiy´ah ni suala linahitaji upambanuzi na haijuzu kusemwa kuwa wao ni sawa na waislamu au ni sawa kabisa. Hili ni kosa. Bali ni suala linahitaji maelezo. Vivyo hivyo Suufiyyah ni makundi na wanahitaji maelezo, si wote wako katika hali moja.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3129/اصناف-الشيعة-والحكم-عليهم
- Imechapishwa: 01/04/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3129/اصناف-الشيعة-والحكم-عليهم
Imechapishwa: 01/04/2026
https://firqatunnajia.com/wanaolingania-umoja-wa-shiyah-na-sunniy-na-kwamba-sote-ni-kitu-kimoja/