Swali: Mwalimu wa kike alikubaliana na mume wake kupanga muda wa kupata mimba na muda wa kujifungua, kiasi kwamba kujifungua kuwe mwanzoni mwa masomo au baina ya ´Iyd mbili ndani ya kipindi cha masomo. Hapana shaka kwamba jambo hilo linasababisha kuvurugika kwa mchakato wa ufundishaji. Je, mshahara wa mwanamke huyu ni halali? Je, wote wawili wanapata dhambi kwa kitendo chao?
Jibu: Haifai kwa mwanamke kutumia vidonge isipokuwa ikiwa kuna haja ya kuvitumia, kwa mfano ikiwa anaathirika kwa kupata watoto mfululizo na hawezi kuwalea ipasavyo. Ama ikiwa hakuna haja, basi haifai kuvitumia. Vilevile ni lazima vidonge hivyo visiwe na madhara. Ikiwa vina madhara, basi havifai.
Kwa hiyo ikiwa vidonge havina madhara na kuna haja ya kuvitumia kwa ajili ya kupanga hedhi wakati wa Ramadhaan, wakati wa Hajj au kwa ajili ya kupanga ujauzito, basi hakuna tatizo. Ama ikiwa hakuna haja ya kuvitumia, basi aviacheni. Aidha ni lazima vidonge hivyo visiwe vya kukata kabisa kizazi wala visiwe na madhara kwa afya. Ama ikiwa matumizi yake ni kwa nia iliyotajwa katika swali, basi watakuwa wamefanya dhambi.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
- Imechapishwa: 30/09/2026
Swali: Mwalimu wa kike alikubaliana na mume wake kupanga muda wa kupata mimba na muda wa kujifungua, kiasi kwamba kujifungua kuwe mwanzoni mwa masomo au baina ya ´Iyd mbili ndani ya kipindi cha masomo. Hapana shaka kwamba jambo hilo linasababisha kuvurugika kwa mchakato wa ufundishaji. Je, mshahara wa mwanamke huyu ni halali? Je, wote wawili wanapata dhambi kwa kitendo chao?
Jibu: Haifai kwa mwanamke kutumia vidonge isipokuwa ikiwa kuna haja ya kuvitumia, kwa mfano ikiwa anaathirika kwa kupata watoto mfululizo na hawezi kuwalea ipasavyo. Ama ikiwa hakuna haja, basi haifai kuvitumia. Vilevile ni lazima vidonge hivyo visiwe na madhara. Ikiwa vina madhara, basi havifai.
Kwa hiyo ikiwa vidonge havina madhara na kuna haja ya kuvitumia kwa ajili ya kupanga hedhi wakati wa Ramadhaan, wakati wa Hajj au kwa ajili ya kupanga ujauzito, basi hakuna tatizo. Ama ikiwa hakuna haja ya kuvitumia, basi aviacheni. Aidha ni lazima vidonge hivyo visiwe vya kukata kabisa kizazi wala visiwe na madhara kwa afya. Ama ikiwa matumizi yake ni kwa nia iliyotajwa katika swali, basi watakuwa wamefanya dhambi.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/wanandoa-wanapata-dhambi-kwa-kutumia-vidonge-vya-kuzuia-mimba/