Swali: Mtu anapokusanya swalah ya Dhuhr na ´Aswr, je, alete Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr kwa swalah zote mbili au anafanya hivyo kwa kila swalah?
Jibu: Inaweza kusemwa kwamba swalah hizo mbili zinaingiliana au achague lililo rahisi kwake. Nimejadili suala hili pamoja na muheshimiwa Shaykh Muhammad bin ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) ambapo akasema kuwa yeye anaposafiri, basi huchagua Dhikr yenye idadi ndogo; mara 33. Kwa maana ya kwamba:
سبحان الله
”Allaah ametakasika na mapungufu.”
mara 11,
الحمد لله
”Himdi zote njema ni za Allaah.”
mara 11
na:
والله أكبر
”Allaah ni mkubwa.”,
mara 11. Jumla inakuwa ni 33. Swalah ya pili anafanya vivyo hivyo mara 33.
Swali: Ikiwa wakati wa Maghrib umeingia na msafiri anataka kufanya kukusanya wakati wa swalah ya ´Ishaa na huku akijua muda atakaokaa baada ya kutoka kwa wakati wa Maghrib, je, inajuzu kwake kufanya hivyo?
Jibu: Maadamu yeye ni msafiri, basi inajuzu kwake kufanya hivyo.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
- Imechapishwa: 30/09/2026
Swali: Mtu anapokusanya swalah ya Dhuhr na ´Aswr, je, alete Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr kwa swalah zote mbili au anafanya hivyo kwa kila swalah?
Jibu: Inaweza kusemwa kwamba swalah hizo mbili zinaingiliana au achague lililo rahisi kwake. Nimejadili suala hili pamoja na muheshimiwa Shaykh Muhammad bin ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) ambapo akasema kuwa yeye anaposafiri, basi huchagua Dhikr yenye idadi ndogo; mara 33. Kwa maana ya kwamba:
سبحان الله
”Allaah ametakasika na mapungufu.”
mara 11,
الحمد لله
”Himdi zote njema ni za Allaah.”
mara 11
na:
والله أكبر
”Allaah ni mkubwa.”,
mara 11. Jumla inakuwa ni 33. Swalah ya pili anafanya vivyo hivyo mara 33.
Swali: Ikiwa wakati wa Maghrib umeingia na msafiri anataka kufanya kukusanya wakati wa swalah ya ´Ishaa na huku akijua muda atakaokaa baada ya kutoka kwa wakati wa Maghrib, je, inajuzu kwake kufanya hivyo?
Jibu: Maadamu yeye ni msafiri, basi inajuzu kwake kufanya hivyo.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/adhkaar-za-ibn-uthaymiyn-wakati-anapokusanya-swalah-mbili/