Swali: Kuna kigezo gani juu ya yale makundi sabini na tatu? Je, wao ni waislamu? Na nini maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yote yako Motoni isipokuwa moja tu.”?

Jibu: Kinachojulikana kwa wanazuoni kuhusu makundi haya ni kwamba wao ni watu wa Bid´ah na kwamba si makafiri. Kuhusu maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yote yako Motoni isipokuwa moja tu.”?

ni katika mlango wa onyo la adhabu ambalo linaweza kumhusu muislamu na kafiri. Kwa mfano muuaji ametishiwa kwa Moto. Aidha mwenye kula mali ya yatima na mla ribaa. Hii ni katika mlango wa vitisho vya adhabu. Si lazima iwe maana ya kwamba kila aliyetishiwa kwa Moto atadumu humo milele.

Kwa sababu hiyo wamesema kwamba Jahmiyyah wako nje ya makundi hayo sabini na mawili, kwa sababu wao ni makafiri. Hivyo hii inajulisha kwamba makundi hayo ni makundi ya wazushi. Haya ndiyo yanayojulikana. Baadhi yao wamesema kwamba miongoni mwao kuna muumini na kafiri.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
  • Imechapishwa: 30/09/2026