Tunasikitika sana kwa kuona kuna watu wenye kujinasibisha na mfumo wa Salaf na wamejivisha mavazi ya Salafiyyah kisha wanawapiga vita vikali wale wenye kushikamana na mfumo huu na kulingania kwayo na kuitetea. Tunawasikitia watu hawa ambao wanawatetea Ahl-ul-Bid´ah walio na Bid´ah kubwa kubwa na kusimama upande wao. Tunamuomba Allaah Awaongoze.

Sisi tunawanasihi: watubu kwa Allaah, washikamane na ukweli na Ikhlaasw. Washikamane na mfumo wa Salaf-us-Swaalih na kuutetea, kutetea watu wake na kumshaji´isha yule mwenye kuwa na mfumo huu na anautetea.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2020