Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy anamfanyia Takfiyr Sayyid Qutwub?

Tuchukulie kuwa Sayyid Qutwub katubu kwa mambo haya – imani ya Wahdat-ul-Wujuud na Huluul – ni kwa nini basi mnatetea na kuvilinda vitabu vyake vilivyojaa upotevu? Ninaapa kwa Allaah lau mngelikuwa mnauheshimu Uislamu basi mngelitutangulia kupiga vita vitabu hivi. Lakini ukweli wa mambo nyinyi ni watu mnaowaabudu watu na madhehebu na hamuiheshimu haki. Ndio maana tunawaona mnatetea vitabu hivi na madhehebu haya machafu haribifu. Mnafanya hivo zaidi ya jinsi mnvotetea Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume wa Allaah na mfumo wa Salaf. Ukiongezea juu ya hilo mnamtetea mtu huyu mpotevu zaidi ya mnavowatetea Mitume, Maswahabah na maimamu wa Salaf. Dalili ya hilo ni kwamba kumtukana kwake Mtume Muusa halikutikisa kitu dini yake, wala ´Aqiydah yake na wala Salafiyyah yake ya uongo. Kadhalika kuwatukana kwake Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Radhiya Allaahu ´anhum) hakukutikisa hata kidogo Salafiyyah hii ya uongo wala ´Aqiydah hii [ya Salafiyyah] wanayodai. Havikutikisa chochote katika hayo wala dhamira yake. Isitoshe, kuukufurishe kwake Ummah mzima, tokea wakati wa Maswahabah mpaka hii leo, hakukutikisa chochote katika hayo.

Pamoja na yote hayo wanadai kwa kutusemea uongo ya kwamba sisi tumemkufurisha mtu huyu. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba, lau ningelimkufurisha lililo la wajibu kwao ilikuwa ni kufunga vinywa vyao. Kwa kuwa hii ni jarima kubwa alofanya: ya kuwatukana Mitume, Maswahabah na kuukufurisha Ummah. Lau wangelikuwa ni wakweli katika dini yao, wenye kutoa nasaha kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi khasira na chuki zao zote wangeliziweka kwa mtu huyu au angalau kwa uchache vitabu vyake. Lakini kinyume chake, chuki na uadui na uongo wao wote wameuweka kwa mtu anayetetea Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume wa Allaah, Mitume wa Allaah, Maswahabah wa Mtume wa Allaah, wanachuoni wa Uislamu na khaswa Ummah wa Kiislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3