Swali: Nakuuliza kuhusu kutikisa kidole cha shahaadah katika swalah, je, kitikiswe mara moja wakati wa Tashahhud au mara nyingi? Kwa sababu nawaona baadhi ya wanaoswali wakitikisa kidole cha shahaadah daima katika swalah yote.
Jibu: Sunnah ni kuashiria kwa kidole cha shahaadah anapokaa katika Tashahhud ya kwanza na ya mwisho. Anakunja vidole vyake vyote na kuashiria kwa kidole cha shahaadah. Wakati mwingine Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakunja kidole kidogo na kidole kinachofuata, na kuunganisha kidole gumba na cha kati kwa mviringo, kisha akaashiria kwa kidole cha shahaadah katika kikao chake cha Tashahhud.
Kuhusu kutikisa kunakuwa wakati wa du´aa, kama ilivyokuja katika Hadiyth:
“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakitikisa anapoomba du´aa.”
Kwa maana wakati wa kuomba du´aa anakitikisa kidogo, kama katika kusema:
اللهم صل على محمد
“Ee Allaah! Msifu Muhammad.”,
أعوذ بالله من عذاب جهنم
“Najikinga kwa Allaah na adhabu ya Moto”,
اللهم أعني على ذكرك
“Ee Allaah nisaidie katika kukutaja.”
na du´aa nyingine mfano wa hizo kabla ya kutoa salamu. Anaashiria kwa kidole chake katika kila du´aa kwa kukitikisa kidogo, kama ilivyokuja katika Sunnah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/296)
- Imechapishwa: 08/03/2026
Swali: Nakuuliza kuhusu kutikisa kidole cha shahaadah katika swalah, je, kitikiswe mara moja wakati wa Tashahhud au mara nyingi? Kwa sababu nawaona baadhi ya wanaoswali wakitikisa kidole cha shahaadah daima katika swalah yote.
Jibu: Sunnah ni kuashiria kwa kidole cha shahaadah anapokaa katika Tashahhud ya kwanza na ya mwisho. Anakunja vidole vyake vyote na kuashiria kwa kidole cha shahaadah. Wakati mwingine Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakunja kidole kidogo na kidole kinachofuata, na kuunganisha kidole gumba na cha kati kwa mviringo, kisha akaashiria kwa kidole cha shahaadah katika kikao chake cha Tashahhud.
Kuhusu kutikisa kunakuwa wakati wa du´aa, kama ilivyokuja katika Hadiyth:
“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakitikisa anapoomba du´aa.”
Kwa maana wakati wa kuomba du´aa anakitikisa kidogo, kama katika kusema:
اللهم صل على محمد
“Ee Allaah! Msifu Muhammad.”,
أعوذ بالله من عذاب جهنم
“Najikinga kwa Allaah na adhabu ya Moto”,
اللهم أعني على ذكرك
“Ee Allaah nisaidie katika kukutaja.”
na du´aa nyingine mfano wa hizo kabla ya kutoa salamu. Anaashiria kwa kidole chake katika kila du´aa kwa kukitikisa kidogo, kama ilivyokuja katika Sunnah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/296)
Imechapishwa: 08/03/2026
https://firqatunnajia.com/wakati-wa-kutikisa-kidole-katika-tashahhud/