Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapowaogopa watu husema:

اللَّهمَّ إنَّا نجعلُك في نُحورِهِم ونعوذُ بِكَ من شُرورِهم

”Ee Allaah! Hakika sisi tunakuweka kwenye koo zao na tunajikinga Kwako kutokana na shari zao.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na an-Nasaa´iy.

Imepokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akisema alipokutana na adui:

اللهُمَّ أَنْتَ عضُدِي وَأَنْتَ نَصِيري بكَ أَحُولُ وَبكَ أَصول وَبك أُقاتلُ

”Ee Allaah! Hakika sisi tunakufanya Wewe uwe katika vifua  vyao na tunajilinda Kwako kutokamana na shari zao.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati  alikuwa katika moja ya vita:

يا مَالِكَ يَوْمِ الدِّينِ إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Ee Mola wa siku ya Malipo! Wewe pekee ndiye tunayekuabudu na Wewe pekee ndiye tunakuomba msaada.”

Anas amesema:

”Hakika niliwaona wanaume wakiangushwa chini na Malaika kutoka mbele yao na nyuma yao.”[3]

Ibn ´Umar ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah amesema:

“Ukipatwa na khofu kwa ajili ya mtawala, au mtu mwingine, basi sema:

لا إِلهَ إِلاَّ اللَّهُ الحَلِيمُ الحَكِيمُ، سُبْحانَ اللَّهِ رَبِّ السَّمَوَاتِ السَّبْعِ وَرَبّ العَرْشِ العَظِيمِ، لا إِلهَ إِلاَّ أنْتَ، عَزَّ جارُكَ، وَجَلَّ ثَناؤُكَ

“Hapana hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Mvumilivu, Mkarimu. Ametakasika Allaah kutokana na mapungufu, Mola wa mbingu saba na Mola wa ´Arshi tukufu. Hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe. Umetukuka ulinzi Wako na zimetukuka sifa Zako.”[4]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

”Allaah  anatutosheleza, Naye ni mbora wa kutegemewa.”[5]

Yamesemwa na Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipotupwa Motoni na yamesemwa na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoambiwa:

إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ

”Hakika watu wamekusanyika dhidi yenu.”[6]

[1] Abu Daawuud (1537) na an-Nasaa’iy katika “´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (601). Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (103), aliyesema kuwa al-Haakim ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

[2] Abu Daawuud (2632) na at-Tirmidhiy (3584), aliyesema kuwa ni nzuri. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (104).

[3] an-Nasaa’iy katika “´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (335). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “al-Kalim at-Twayyib”, s. 121.

[4] an-Nasaa’iy katika “´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (340). Dhaifu sana kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “al-Kalim at-Twayyib”, uk. 121.

[5] 3:173

[6] 3:173 al-Bukhaariy (4563).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 300-302
  • Imechapishwa: 10/09/2025