Wakati (الدهر) ni jina la Allaah?

Swali: Je, wakati ni katika majina ya Allaah?

Jibu: Hapana, Yeye ndiye Muumba wa wakati. Wakati ni zama. Allaah ndiye muumba wake. Ndio maana Allaah (Jalla wa ´Alaa) akasema:

”Naugeuza usiku na mchana wake.”

Swali: Lakini amesema kuwa Mimi ndiye wakati?

Jibu: Hii ina maana kwamba Mimi ndiye Muumba wa wakati, kama ilivyo katika Hadiyth:

”Naugeuza usiku na mchana wake.”

Swali: Je, sio katika sifa za Allaah?

Jibu: Hapana, wakati ni kitu kilichoumbwa, ni zama.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24660/هل-الدهر-من-اسماء-الله-تعالى
  • Imechapishwa: 20/11/2024