Wajibu wako unapomuona mwanaume anayeingia nyumbani kwa mwanamke

Swali: Je, inafaa kwa mtu kunyamaza ikiwa anajua kuna bwana ambaye anazini na mwanamke au anaingia nyumbani kwa mwanamke mpaka pale Allaah atapomfichua?

Jibu: Hapana, huku ni katika kukemea maovu. Haijuzu kwake kunyamaza. Ikithibiti kuwa anaingia kwa mwanamke wakati ambapo walii wake hayupo, aende kushtaki kwa maafisa wa mapolisi wa kidini ambao watamfuatilia na kumtega na baadaye kumkamata.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (46)
  • Imechapishwa: 11/08/2024