Swali: Uchawi unawapata waja wema ambao wanachunga Adhkaar na nyuradi za kila siku?

Jibu: Uchawi unaweza kumpata mtu. Lakini mwenye kushikamana na kamba ya Allaah, akajilinda kwa maneno ya Allaah timilifu kutokana na shari ya alivyoviumba na akaomba zile du´aa za kinga kwa mujibu wa Shari´ah, basi hakika Allaah (Jalla wa ´Alaa) atamlinda.

Swali: Ni vipi tutaonisha ya kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanyiwa uchawi ilihali ndiye mbora wa watu?

Jibu: Inaweza kuwa ni kwa sababu alikutana na jambo ambalo halina kinga, alikutana na siku au saa ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya sababu ya kujilinda.

Swali: Je, ilikuwa ni kabla ya kuteremshwa al-Falaq, an-Naas na al-Ikhlaasw?

Jibu: Inawezekana. Allaah ndiye mjuzi zaidi. Ni wajibu kwa muumini kupupia juu ya kinga zilizowekwa katika Shari´ah na juu ya zile Suurah za ulinzi ambazo Allaah ameweka katika Shari´ah. Pengine kwa kufanya hivo Allaah (Jalla wa ´Alaa) akamtosheleza na shari.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24602/هل-يصاب-الصالحون-بالسحر
  • Imechapishwa: 08/11/2024