Vitu ambavyo watu wanaegemea juu yake wakati wa swalah

Swali: Miongoni mwa mambo yenye kuonekana kwenye misikiti mingi ni kupatikana kwa vitu mbalimbali katika safu ya kwanza ambavyo wanaegemea wale waswaliji wakati wanaposubiri kuswali au baada ya swalah. Lakini tunawaona baadhi kwamba wanaegemea juu yake wakati wanaposimama na kurukuu kwa miundi yao ndani ya swalah. Baadhi yao wanafanya hivo katikati ya Tashahhud ambapo wanaegemea kwa migongo yao. Je, matendo yao haya ni sahihi?

Jibu: Sioni kama kuna neno juu ya vitu vya kukaliwa na kuegemea. Kwa sharti iwe urahisi kukitambuka. Kwa sababu baadhi ya vinavyo ikaliwa na kuegemewa vinainuliwa hadi vinaleta uzito kwa yule anayetaka kuvivuka. Kikiwa ni kifupi hakileti uzito kwa yule anayetaka  kukivuka hakuna ubaya.

Kuhusu kuegemea juu yake wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kwamba iwapo mtu ataegemea kwenye nguzo – kuegemea kikamilifu kwa kiasi cha kwamba endapo nguzo hii itaondoshwa ataanguka – basi swalah yake ya faradhi haisihi. Kwa sababu hakusimama kisimamo ambacho ametegemea viungo vyake. Ama ikiwa anafanya hivo katika hali ya kukaa kwake chini hakuna neno akaegemea juu yake japokuwa itakuwa ni kuegemea kikamilifu. Lakini hata hivyo kuegemea kwake juu ya viungo vyake ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (68) http://binothaimeen.net/content/1539
  • Imechapishwa: 19/02/2020