Swali: Ni vitabu vipi unavyopendekeza na ni vitabu vipi unavyotahadharisha?
Jibu: Napendekeza Qur-aan, Sunnah na vitabu vyote vya Salaf, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa jumla. Havihesabiki. Atakayevifanya ni vyanzo juu ya dini na elimu yake atatosheka navyo. Hahitajii vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah.
Tunatahadharisha vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal; vitabu vya Suufiyyah, vitabu vya Khawaarij, vitabu vya Raafidhwah, vitabu vya al-Ikhwaan al-Muslimuun, vitabu vya Qutbiyyuun. Vyote hivi ni vitabu vya Bid´ah na upotevu. Tunawatahadharisha vijana wa Ummah navyo. Vivyo hivyo inahusiana na kaseti za watu hawa inayoenda kinyume na mfumo wa Salaf. Anayetaka kulelewa juu ya mfumo wa Allaah wa haki na mfumo wa Salaf basi atambue kuwa vyanzo vyake vimejaa. Uhai wote wa mtu unaweza kwenda na mtu asijaaliwe kuvipitia vyote.
Ni kipi kinachomvutia na vitabu vya wapotevu? Tangu ile siku ya kwanza ataanza kufuata vitabu vya wapotevu. Hoja yake ni kuwa anaweza kupambanua kati ya haki na batili; anadai kuwa anachukua yale ambayo ni haki na anaacha yale ambayo ni batili. Mwishowe anachukua yale ambayo ni batili na anaacha yale ambayo ni haki. Haya yamewapitikia watu wengi.
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 20
- Imechapishwa: 06/11/2016
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)