Swali: Kuhusu kujitenga na Mkusanyiko inakuwa kwa vitendo na maneno au ni kwa vitendo pekee?

Jibu: Ni kwa maneno, vitendo na imani. Ni lazima mtu awe pamoja nao katika imani, maneno na matendo; asijitenge nao wala kuwapinga katika mambo hayo, bali awe miongoni mwa wanaowaunga mkono.

Swali: Je, wendaji kinyume unakuwa katika jambo ambalo kuna maafikiano juu yake?

Jibu: Unakuwa katika haki, ni mamoja iwe ni jambo kuna maafikiano juu yake au sivyo. Kila lililo na dalili ni wajibu kuthibiti juu yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31150/كيف-تكون-مفارقة-الجماعة
  • Imechapishwa: 09/10/2025