Vifungo vya maiti anapolazwa ndani ya kaburi

Swali: Je, lililo bora ni kulegeza vifungo vilivyoko kwenye kichwa cha maiti na kuacha vile vilivyo kwenye miguu yake na katikati au vifuguliwe vyote?

Jibu: Vifungo vinavyofungwa kwenye sanda vifunguliwe vyote. Kufanya hivo ndio bora. Sunnah ni kufunguliwa vyote kaburini. Akiwekwa kaburini hufunguliwa vifungo vyote, vya mwanzo na vya mwisho. Hii ndiyo Sunnah. Vifunguliwe na vibaki mahali pake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1021/حكم-حل-عقد-الكفن-عند-وضع-الميت-في-قبره
  • Imechapishwa: 24/12/2025