Uwajibu wa wanazuoni na walinganizi kutahadharisha dhidi ya Shiy´ah

Swali: Haifichiki kwa muheshimiwa wenu harakati ambazo Shiy´ah wamezifanya katika kuwakumbusha watu dini, kwani katika wakati huu zimeongezeka sana, khaswa katika Indonesia, Malaysia, Thailand na Ufilipino, na khaswa Afrika ambayo hapo awali haikuwa na madhehebu ya Shiy´ah. Idadi ya Shiy´ah katika bara la Afrika imefikia mamia ya maelfu na wameacha Sunniy katika nchi tulizozitaja. Harakati zao zimeongezeka katika kueneza madhehebu ya Shiy´ah katika nchi nyingi ambazo hatuwezi kuzihesabu. Kwa hiyo nafasi ya wanazuoni katika kulingania kwa Allaah na uongofu ni kubainisha ´Aqiydah ya Shiy´ah na ubaya waliomo ndani yake. Tunakujulisheni pia kuwa wengi wanaowadanganya waislamu wanawatangazia na kusema kwamba hakuna tofauti kati yetu na wao. Hii ndiyo sababu ya kuwabadilisha Sunniy kuwa Shiy´ah. Ulingano wao umeanza kuenea kwa watu kwa njia ya siri. Tunaomba kutoka kwenu jibu na kutenga mihadhara ya kubainisha ´Aqiydah ya Shiy´ah.

Jibu: Jambo hili alilotaja muulizaji limefika kwetu, limejulikana na limeenea. Imekuwa ikijulikana hali ya Shiy´ah Raafidhwah wanaoitwa kundi la Ithna ‘Ashariyyah, na pia huitwa Ja‘fariyyah na pia Imaamiyyah, khaswa baada ya kuongoza kwa kiongozi wao Khumayniy, shari yao imeenea na imeonekana katika maeneo mengi.

Walinganizi na wanazuoni wanaohesabiwa kuwa ni wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah wameitambua hali hii, wameendelea kupambana na madhehebu ya Shiy´ah, kuwaonya watu juu ya khatari yake, kwamba ni Bid´ah mbaya, njia inayopelekea shirki kwa Allaah, kuwatukana Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), kumuabudu al-Husayn na kurudi kwa kuabudu mizimu. Hili ni jambo linalojulikana. Wanazuoni mashuhuri wako macho juu yake, pia walinganizi na wale wanaohusiana na idara za fatwa na mashirika ya Kiislamu wana elimu ya jambo hili. Wana – kwa fadhilah za Allaah – na juhudi ambazo tunatarajia Allaah azifanye ziwe na manufaa kwa ummah.

Wajibu juu ya wanazuoni, wanaolingania katika Tawhiyd na Sunnah kila mahali – ni mamoja wawe ni wafanyakazi au si wafanyakazi – ni kuongeza juhudi zao katika kueneza Sunnah na kupinga Bid´ah zote, khaswa Bid´ah hizi. Wawe na juhudi katika Khutbah za ijumaa, katika mawaidha yao yote na katika hali zao zote, khaswa katika nchi ambazo Shiy´ah wapo na wana ulingano, kupitia njia za balozi au njia nyingine. Hii ndiyo njia ya kujilinda na shari yao na kuwatahadharisha waislamu dhidi ya Bid´ah hii mbaya. Hakuna shaka kuwa ni wajibu kuongeza juhudi – kutoka kwetu na kutoka kwa wengine – katika jambo hili.

Ulingano wa Shiy´ah wa Khumayniy, Raafidhwah, Imaamiyyah, Ja‘fariyyah ni ulingano mbaya sana, kwani inaita kwenye mambo mengi mabaya ikiwa ni pamoja na kuwatukana Maswahabah, kuwalaani Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan, kudai kuwa uongozi wao ni batili na walimdhulumu ´Aliy, kuwatukana Maswahabah wengi na kuwatuhumu kuwa waovu au makafiri. Ikiwa Maswahabah ambao walibeba Sunnah na Shari´ah wanahesabiwa kuwa waovu au makafiri, basi Shari´ah itakuwaje? Hili ni katika maovu makubwa na ufisadi mkubwa duniani. Tunajikinga kwa Allaah.

Kadhalika wanadai kwamba maimamu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), khaswa ´Aliy, wanajua ghaibu, wamekingwa na kukosea, kwamba inajuzu kuwaomba badala ya Allaah, kuomba msaada kwao na kuweka nadhiri kwao. Yote haya ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na ni ukafiri mkubwa.

Hivyo ni wajibu kwa wanazuoni kufahamu hali yao kwa undani, kuwa na uelewa sahihi popote walipo ili wawabainishie watu uovu huu na kuwatahadharisha nao ili shari yao isiene Afrika wala sehemu nyingine. Kadhalika katika baadhi ya maeneo kama mashariki kuna uwepo wao na pia katika baadhi ya maeneo mengine kama Madiynah kuna kiasi fulani.

Kwa hiyo ni wajibu kwa wanazuoni kubainisha jambo hili, kuwalingania watu kufuata Sunnah na kuitukuza na wasifuate wanazuoni wa Shiy´ah waliopotea katika jambo hili khatari.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3143/الواجب-نحو-ازدياد-نشاط-الشيعة-في-دعوتهم
  • Imechapishwa: 01/04/2026