Usikunje nguo zako kabla ya swalah

Swali: Hadiyth inasema:

“Nimeamrishwa kusujudu juu viungo saba na nisikunje nguo.”[1]

Je, Hadiyth ni Swahiyh? Nini maana yake?

Jibu: Hadiyth hii ni Swahiyh. Makusudio ni kwamba asikunje nguo wakati wa kuswali. Kinachotakiwa kwa mswaliji ni kwamba azibakize nguo zake kama zilivyo. Asizikunje na baadaye akazinyanyua kutoka ardhini, na wala asikunje pia mikono yake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimeamrishwa kusujudu juu viungo saba na nisikunje nguo.”

[1] al-Bukhaariy (810) na Muslim (490).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/305)
  • Imechapishwa: 03/04/2026