Swali: Ikiwa atanialika kwenye walima mtu anayejulikana kuwa anaacha swalah, je, nimuitikie? Je, analiwa mnyama aliyemchinja mtu anayeacha swalah?
Jibu: Ikiwa anayekualika unamjua kuwa anaacha swalah, basi usiitikie mwaliko wake. Ni wajibu kutokuitikia mwaliko wake. Anayejua hali yake anapaswa kumnasihi, kumuamrisha mema na kumkataza maovu. Akitubu, basi ni vyema, na asipotubu, basi ni wajibu kumshtaki kwa wenye mamlaka, kwa vyombo husika au kwa kiongozi wa eneo. Wala haijuzu kumuacha bila kukemewa. Anapaswa kuanza kwa nasaha na maelekezo, kumuamrisha mema, kumtahadharisha na matokeo mabaya ya kitendo chake na kubainisha kwamba kuacha swalah ni katika ukafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ahadi iliyopo baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi yule mwenye kuiacha amekufuru.”
Ameipokea Imaam Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaaiy na Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kupiita kwa Buraydah (Radhiya Allaahu ´anh).
Muslim amepokea katika ”as-Swahiyh” kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kati ya mtu na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”
Kwa hivyo kuacha swalah ni sababu ya kuingia katika ukafiri mkubwa kwa mujibu wa maoni yaliyo na nguvu zaidi ya wanazuoni.
Wanazuoni wengine wamesema ni ukafiri mdogo. Lakini sahihi ni kuwa ni ukafiri mkubwa ikiwa mtu anaacha kwa makusudi huku akijua hukumu. Ama yule aliyeacha kwa kusahau au kwa usingizi, huyo anapaswa kulipa swalah mara tu anapokumbuka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]
Kuhusu anayeliacha kwa makusudi, basi ni wajibu kwa waislamu kumhama, kumkemea, kutomtembelea, kutomtembelea akiwa mgonjwa, kutokuitikia mwaliko wake, kutomualika na kutokukaa naye. Bali aepushwe mpaka Allaah amuongoze na kutunukiwa tawbah au adhibiwe kwa hukumu inayostahiki. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ
“Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waachilieni huru.” (09:05)
Kwa hiyo ikafahamisha ya kwamba asiyeswali haiachwi huru njia yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hakika mimi nimekatazwa kuwaua wanaoswali.”
Kwa hiyo ikafahamisha ya kwamba asiyeswali haizuiwi kumuua. Kinyume chake kunaamrishwa kuuawa. Anatakiwa kuambiwa kutubia. Akitubia ni vyema. Vinginevyo auliwe hali ya kuwa ni kafiri kwa mujibu wa maoni sahihi. Wanazuoni wengine wamesema kuwa atauliwa hali ya kuwa ni mtenda dhambi. Hata hivyo dhambi yake haifikii kiwango cha ukafiri mkubwa. Hata hivyo maoni ya kwanza ndio sahihi; ya kwamba ni kufuru kubwa.
Swali: Je, huliwa kichinjwa chake?
Jibu: Hakiliwi kichinjwa chake, kwa sababu ni kafiri.
[1]al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3190/حكم-اجابة-دعوة-تارك-الصلاة-للوليمة
- Imechapishwa: 02/11/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3190/حكم-اجابة-دعوة-تارك-الصلاة-للوليمة
Imechapishwa: 02/11/2026
https://firqatunnajia.com/usiitikie-mwaliko-wa-asiyeswali/