Upande wa Qiblah uko makosa kwa digrii tatu

Swali: Qiblah cha msikiti wetu umekengeuka, kwa mujibu wa dira, kwa digrii tatu. Watu wengi wanaswali kwa kuelekea upande huo kwa sababu walikuwa hawajui kuwa kimepinda. Je, ukengeukaji huu unaathiri kusihi kwa swalah? Je, ni wajibu kuurekebisha msikiti?

Jibu: Ukengeukaji mdogo kwa njia ya kwamba bado mtu anaswali kwa kuelekea Qiblah haudhuru. Licha ya kuwa hapana shaka yoyote kuelekea usawa ndio bora zaidi. Lakini ikiwa ukengeukaji ni mkubwa kwa namna kwamba akaelekea upande wa kusini na Qiblah kiko upande wa mashariki, au akaelekea kaskazini na Qiblah kiko upande wa mashariki, au akaelekea mashariki na Qiblah kiko upande wa kusini, basi hapana shaka kwamba ni lazima kuurekebisha msikiti au kuswali kwa kuelekea upande sahihi wa Qiblah hata kama itakuwa ni tofauti na mwelekeo wa msikiti.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/414)
  • Imechapishwa: 18/04/2026