Upambanuzi juu ya kutumia vidonge vinavyozuia ada ya mwanamke

Swali: Mwanamke kupenda sana kheri kunaweza kumpelekea akafanya baadhi ya vitu vinavyozuia ada ya mwezi ili aweze kufanya ´Umrah, kufunga au kuswali Ramadhaan. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Asivitumie kwa minajili ya kuswali Ramadhaan au kufunga Ramadhaan. Kwa sababu jambo lina wasaa na himdi zote anastahiki Allaah. Hiki ni kitu ambacho Allaah amewaandikia wasichana wa Aadam. Hivo ndivyo alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Nimefikiwa na khabari kutoka kwa madaktari waaminifu na wakweli kwamba vidonge hivi vina madhara makubwa.

Kuhusu kufanya ´Umrah huenda akaruhusiwa. Kwa sababu katika kufanya ´Umrah kuna tatizo; itampita iwapo hedhi itamjia wakati wa Ihraam kabla ya kufanya Twawaaf na akarudi nyuma kabla ya kutufu. Hapa kuna tatizo. ´Umrah huenda akaruhusiwa. Ama kwa ajili ya kufunga, kuswali na kusoma Qur-aan hapana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1636
  • Imechapishwa: 28/03/2020