Kwa hivyo moja katika nasaha kwa wanazuoni wa waislamu ni kutetea heshima zao na kuzisitiri kadiri na uwezavyo. Usinyamaze pale utaposikia uvumi. Mzindue mwanachuoni huyo na ufanye upelelezi pamoja naye na kumuuliza. Pengine kukanukuliwa mambo kutoka kwake yasiyokuwa sahihi. Kumenukuliwa mambo kutoka kwangu na kwa wengine yasiyokuwa sahihi. Lakinia hata hivyo watu wanapokuwa na matamanio yao na kutaka jambo na wakajua kuna mwanachuoni ambaye watu wanakubali maneno yake wanamnasibishia mambo hayo mwanachuoni huyu. Halafu ukimuuliza mwenyee hayo aliyonasibishiwa anayakana na kwamba hakuyakusema. Vilevile kuna uwezekano muulizaji akakosea namna vile anavouliza na matokeo yake mwanachuoni huyo akajibu vile swali lilivo na muulizaji akaelewa kutegemea na kile kilichomo ndani ya nafsi yake. Hivyo kukatokea makosa. Kadhalika kuna uwezekano mwanachuoni akajibu kwa usawa baada ya kufahamu swali lakini hata hivyo muulizaji akafahamu kimakosa na matokeo yake akakosea katika kunukuu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/394-395)
- Imechapishwa: 29/07/2025
Kwa hivyo moja katika nasaha kwa wanazuoni wa waislamu ni kutetea heshima zao na kuzisitiri kadiri na uwezavyo. Usinyamaze pale utaposikia uvumi. Mzindue mwanachuoni huyo na ufanye upelelezi pamoja naye na kumuuliza. Pengine kukanukuliwa mambo kutoka kwake yasiyokuwa sahihi. Kumenukuliwa mambo kutoka kwangu na kwa wengine yasiyokuwa sahihi. Lakinia hata hivyo watu wanapokuwa na matamanio yao na kutaka jambo na wakajua kuna mwanachuoni ambaye watu wanakubali maneno yake wanamnasibishia mambo hayo mwanachuoni huyu. Halafu ukimuuliza mwenyee hayo aliyonasibishiwa anayakana na kwamba hakuyakusema. Vilevile kuna uwezekano muulizaji akakosea namna vile anavouliza na matokeo yake mwanachuoni huyo akajibu vile swali lilivo na muulizaji akaelewa kutegemea na kile kilichomo ndani ya nafsi yake. Hivyo kukatokea makosa. Kadhalika kuna uwezekano mwanachuoni akajibu kwa usawa baada ya kufahamu swali lakini hata hivyo muulizaji akafahamu kimakosa na matokeo yake akakosea katika kunukuu.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/394-395)
Imechapishwa: 29/07/2025
https://firqatunnajia.com/unaposikia-maneno-yenye-kutia-shaka-ya-mwanachuoni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket