Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema kuhusu kisa cha wale mabwana wawili:
وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ
“Na lau ulipoingia bustanini mwako ungelisema: ‘Ametaka Allaah, hapana nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah´!”[1]
Yeyote anayeingia kwenye bustani yake au nyumba yake, au akaona kitu kinachompendeza katika mali na familia yake, basi anatakiwa papo hapo kusema maneno haya, kwani hatoona kitu kibaya hapo.
Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Allaah anapomneemesha mja katika familia, mali au watoto, ambapo akasema:
ما شاء الله لا قوة إلا بالله
”Kama alivyotaka Allaah! Hapana nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah!”,
isipokuwa hatoona wanapatwa na msiba wowote mdogo isipokuwa kifo.”[2]
Huyohuyo (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza tena ya kwamba alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema wakati anapoona kinachompendeza:
الـحَمْدُ للـهِ الَّذِي بِنِعْمَتهِ تَتِمُّ الصَّالِـحَاتُ
”Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye kwa neema Zake yanatimia mazuri.”
Anapoona kitu kinachomchukiza husema:
الـحَمْدُ للـهِ عَلَى كُلِّ حَالٍ
”Himdi zote njema anastahiki kwa hali zote.”[3]
[1] 18:39
[2] at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” (4/301). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (5026).
[3] Ibn Maajah (3803) na al-Haakim (1/499), ambaye ameisahihisha.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 305-306
- Imechapishwa: 08/09/2025
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema kuhusu kisa cha wale mabwana wawili:
وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ
“Na lau ulipoingia bustanini mwako ungelisema: ‘Ametaka Allaah, hapana nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah´!”[1]
Yeyote anayeingia kwenye bustani yake au nyumba yake, au akaona kitu kinachompendeza katika mali na familia yake, basi anatakiwa papo hapo kusema maneno haya, kwani hatoona kitu kibaya hapo.
Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Allaah anapomneemesha mja katika familia, mali au watoto, ambapo akasema:
ما شاء الله لا قوة إلا بالله
”Kama alivyotaka Allaah! Hapana nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah!”,
isipokuwa hatoona wanapatwa na msiba wowote mdogo isipokuwa kifo.”[2]
Huyohuyo (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza tena ya kwamba alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema wakati anapoona kinachompendeza:
الـحَمْدُ للـهِ الَّذِي بِنِعْمَتهِ تَتِمُّ الصَّالِـحَاتُ
”Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye kwa neema Zake yanatimia mazuri.”
Anapoona kitu kinachomchukiza husema:
الـحَمْدُ للـهِ عَلَى كُلِّ حَالٍ
”Himdi zote njema anastahiki kwa hali zote.”[3]
[1] 18:39
[2] at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” (4/301). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (5026).
[3] Ibn Maajah (3803) na al-Haakim (1/499), ambaye ameisahihisha.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 305-306
Imechapishwa: 08/09/2025
https://firqatunnajia.com/unapopata-neema-mpya-na-kutaka-kuihifadhi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket